JUKUMU LA MUISLAM KUELEKEA KATIKA UCHAGUZI MKUU OKTOBA, 2025
Uislam umempa fursa Muislam kushiriki katika masuala yote yanayohusu maisha yake ya kila siku bila kuvunja Sheria za dini ya kiislam, hayo yapo wazi katika mafundisho mema ya Mtume Muhammad (S.A.W) aliposema (tenda kwa ajili ya dunia yako kama utaishi milele na tenda kwa ajili ya akhera yako kama utakufa kesho) hivyo raia Muislam anayo haki kama raia wengine ya kushiriki uchaguzi na ana haki kama Muislam kushiriki kwa kuwa uislam haumkatazi kufanya hivyo.
Wajibu wa pili ni kulinda amani ya Nchi yake na kuhakikisha amani hiyo inaendelea sababu ya kufanya hivyo ni ukweli usiofichika. Kwamba, ibada ili ifanyike vizuri inahitaji mazingira ya utulivu, bila utulivu huwezi kupata mazingira mazuri ya ibada hivyo muislam anatakiwa kutoshiriki katika uvunjifu wa amani ama kuwa sababu ya kuwasaidia wanaolenga kuvunja amani ya Nchi.
Aidha, ni sunna ya Mtume wetu kuipenda Nchi ama Mji, Mtume amesikika akisema (kupenda Nchi ni katika alama za kukamilika kwa Imani ya Muumin) sisi kama Waislam wa Tanzania ni wajibu wetu kuhakikisha amani inaendelea nchini kwa kuwa Tanzania
ndio nchi yetu na hatuna Nchi nyengine ya kujivunia zaidi ya
Tanzania.
Hivyo ni wito wangu kwa jamii ya Waislam nchini tushiriki uchaguzi ujao na tuhakikishe tunawachagua viongozi waadilifu na tujiepushe na kufanya vitendo vya kuharibu Amani.
0 Comments