KUISHI KWA AMANI NA KILA MWANADAMU KWA MUJIBU WA QURAN
Tangu Mwenyezi Mungu alipomshusha Adam katika ardhi basi Manabii na Mitume wamekuja kizazi baada ya kizazi kwa dini za mbinguni ili kuwageuza watu kutoka gizani na kuelekea kwenye mwanga ili watu wapate usalama, furaha na uwongofu wao.
Kwa hakika dini zote za mbinguni zimekubaliana kuwa ni dini zilizotelemshwa na Mwenyezi mungu. Na malengo yake ni kuhakikisha utumwa wa kweli kwa Mwenyezi Mungu peke yake, na uihuisha ardhi kwa mujibu wa mbinu ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo uislamu unakubaliana na dini nyingine zilizoteremshwa kabla yake kama vile ukristo kwa mfano kuhusu misingi hiyo na mingine kama vile huruma, uadilifu, usawa uhuru ushirikiano na maadili mema.
Pia, uislamu umeashiria kwamba machimbuko ya ubinadamu ni moja na hatatofautiani kwa rangi, makabila au lugha, Mwenyezi Mungu (S.W.) amesema "Enyi watu, Mcheni Mola wenu mlezi aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao mwanamme na wanawake wengi" (al -nisaa: 1).
Uislamu umebainisha kuwa kuna nafasi ya kutosha ya kuishiana na wengineo kwa uadilifu na ihsani, Mwenyezi Mungu amesema "Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, hawakukutoeni makwenu" (Al- Mutahanah: 8). Na wakati alipohama Mtume (SA.W.) kutoka makkah kuelekea Madina na akaanza kuunda mfumo wa nchi ya kiislamu iliyotanda mpaka aghalabu iliyokuwa inakusanya makundi mengi kama vile Al-Mhajiriin, Mayahudi na wengineo.
0 Comments