UMUHIMU WA KUTUNZA AMANI NA UTULIVU KATIKA JAMII NA NCHI KWA UJUMLA
MWENYEZI MUNGU muumba wa mbingu na ardhi ndiye ambaye anatakiwa kushukuriwa kwa haki kwa kuendelea kutubariki kwa uzima na afya.
Katika jamii yeyote naNchi kwa ujumlaili kuwepo kwamaendeleo ni muhimu kwa kila mmoja kuhakikisha kuna Amani na utulivu. Kwa kuwa jamii inaundwa na binadamu na uwepo wa binadamu huyo ni muhimu,hivyo ni lazima kuwepo kwa azma ya dhati kwa kila mmoja kuhakikisha kuna amanina utulivukatika jamiiinayomzunguka ili kuweza kuzuia machafuko na uvunjifuwa amani unaoweza kutokea katika jamii.
Jamii zote zimejengwa na binadamuwenyeitikadi, Imani, fikrana mtazamo usiofanana katika nyanjaza siasa, dini na kabila. Kadhalika, hali hiyo ipokwa mwanadamu kutokana na maumbile ya mwanadamu mwenyewe.
Hata hivyo katika maandiko mbalimbali matukufuya Mwenyezi Mungu (S.W) aya ya 1 katika Suratal Nisaiimeeleza kuwa “kwa hakika sisitumekuumbeni kutokana na mwanaume mmoja na mwanamke mmoja na tukakujalienimataifa na makabila mbalimbali ili mjuane ,hakika ubora wenu mbele ya Allah niyule mchaji zaidi”.
Aya hii imehimiza umoja na upendomiongoni mwa wanadamu ambapo itapelekea kuwepo kwahali yaamani na utulivukatika jamii na Taifa kwa ujumla.
Utulivu na amanini muhimu katika kuwezesha maendeleoendelevuila ikiwa kinyume chake kamailivyo kuwepokwa hali ya ghasiaitakuwa ni mojaya vikwazovikubwavyamaendeleo hayo. Itakuwa ni jambo la kutia moyo na muhimuendapo mapigano na vita vitapungua katika dunia kwakuwa uwepo wamigogoro na vita husababisha maafamakubwa yakiwemo vifo na ulemavu kwa watuvile inapokosa amanina utulivumigogoro na fujo ndio hushika hatamu na jamii huporomokakatika kilanyanja mbele ya jamii nyingine.
Katika aya ya 46 Surat al Anfal Mwenyezi Mungu ameeleza kuwa“ Wala ,msizozane , msigombanemsijemkaharibikiwanakupotezanguvu zenu , navumilienimstahimilienibilashaka Mwenyezi Mungu yupo pamojana wanaovumilia” aya hii bado inahimiza umuhimu wa kudumisha Amani na utulivu pamoja na kuwa na uvumilivu.
Vile vileili kufikia lengo kuu la kutokemeza umaskinikutabakia ndoto kwa wengiiwapo jamii haitashirikianakumalizamigogoro naukosefu wa utulivu, ikijumuisha uwepokwa uongozi bora , utawalawa kisheria, haki za binadamuna haki ya maendeleo kwa wote.
Katika muktadha wa dini, uadilifu , uvumilivu huwaunanyanyua utu wa mtu mbele ya watu wengine , kabila , dini , ukoo na Taifa kwa ujumla . Pia dini inasisitiza tabia njema na inatukataza kuwafanyia watu wengine matendo maovu ikiwemo kuwadharau, kuwanyanyasa, sababu hali hiyo itasaidia kudumisha amanina utulivu kwa jamii nzima.
Mbali na dini kuhimiza kudumisha amani na utulivu vile vile kwa upande waNchi husika kupitia katibazao zimetoamiongozo kwa Serikali, Taasisi na Vyama katika kudumisha na kutetetahakina usawa kwa binadamu wote, hatua hiiitasaidia kuhimiza kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kudumisha na kulinda amani na utulivu katika jamii aliyopo.
Amani na utulivu katika jamii na Nchi kwa ujumla ni tunu ambayo inatakiwa kulindwakwa namna yeyote ile , hivyoilikuyafikia mafanikio ya kuwa na amani na utulivu ni lazima kila mmoja kutekeleza wajibu wake mahali pale alipo kwa maana athari ya uvunjifu wa amani ni kubwa na hatari kwa mustakabali wa jamii na Taifa kwa ujumla .
Wito wangu kwa watanzania na dunia kwa ujumla ni muhimu kuchukuliwa hatua kali kwa mtu au kikundi chochote cha watu ambao wataonekana kwa makusudi wanataka kuvuruga amani na utulivu katika jamii na Nchi, tushirikiane kulinda amanina utulivu wa Nchi yetu.
1 Comments